VIONGOZI WA PAROKIA

VIONGOZI WA PAROKIA

Sunday 29 March 2015

JUKWAA LA VIJANA


Hii ni sehemu au ulingo (platform) ulio huru wa vijana hasa wa Ubungo Msewe kukaa chini na kuzungumzia masuala ambayo yataleta chachu kuwaendeleza kiuchumi,kijamii na kiroho katika mahali wanamoishi.
Tumezoea sana vijana wengi wanakuwa wakitegemea ajira pekee kama sehem ya kujipatia kipato kumbe wanasahau wanaweza kujiendeleza wenyewe kwa kufanya shughuli za kijasiriamali.
Hivyo kila kijana katika parokia ya Ubungo Msewe ana wajibu wa kuwa sehem ya hili jukwaa na kuleta mawazo yake chanya kwa maendeleo ya vijana wote.
Jukwaa hili litafanyika kila jumapili ya mwisho wa mwezi na litakuwa likisimamiwa na Spika Frank Kondo na Msaidiz wake Albert Msamia huku likiwezeshwa na mlezi kaka Charles ........
Uongozi wa vijana parokia utajitahidi kufanya jukwaa hili kila Juma Lpili ya mwisho wa mwezi vijana wote mnaombwa msikose.
Imeandikwa na Spika wa jukwaa Frank Kondo
Akisaidiana na Albert Msamila naibu Spikaa

ILIVYOKUA JANA KATIKA MAFUNGO VIJANA PAROKIA PUGU tarehe28-3-2015

Picha ya pamoja ya vijana wacchache walio udhuria wakiwa katika msalaba ulioko katika msitu wa biblia ya ardhini.

CHUKUA MDA WAKO KUANGALIA PICHA ZOTE KWENYE KILA SLIDE ZIKO ZAIDI YA200
            

Slide hapo juu zina onesha SEMINA na IBADA kama tulivyoogozwa na Padre CALISTI alitufudisha mengi sana mada kuuilikua ni DHAMIRA YA MWANADAMU.
Jisi yakutambua DHAMIRA inayo faa na isio faa.
Hivi ndivyo ilikua tulivyoenda kutembelea biblia ya ardhini kwanzia kitabu cha MWANZO hadi UFUNUO WA YOHANE. Pia kulikua na picha zamafundisho mbalimbali ya kiroho na kiimani zaidi kweli pata kitu kikubwa sana huko.
MAPENDOOO......
picha na #deomkawe


Thursday 19 March 2015

MATCH DAY THIS SUNDAY 22-3-2015

Jumapili hii tarehe 22-03-2015 mida ya saa9 jioni katika viwanja vya EBONITE COLLEGE Vijana wa kigango cha GOLANI watachuana vikali kabisa na vijana wa kigango cha BARUTI.
Mtanange huo ambao utahusisha mamluki kama Msuva wa Simba B na wengine wengi utanogeshwa na burudani toka vikundi mbali mbali vya vijana Parokia.
MATCH
VIJANA KIGANGO CHA GOLANI vs VIJANA KIGANGO CHA BARUTI

Saturday 14 March 2015

VIJANA KATIKA MATENDO YA HURUMA WAMEMTEMBELEA BIBI YAKE YULIA MLOWE

Vijana wa parokia ya Msewe wakiongozwa na mwenyekiti wa parokia Fransi Haule na mwenyekiti wa kigango cha Msewe baada yakutoka kwenye hija BOKO walienda mpaka nyumbami kwa bibi Yulia Mlowe kumpa pole bibi yake mpenzi aliefanyiwa operesheni wiki chache zilizo pita.
Kutembelea wagonjwa ni moja ya utume muhimu wa vijana wa parokia ya Ubungu Msewe Mungu awabariki wote walio fika kumpa pole bibi Yulia Mlowe..
MAPENDOOO......
Picha na #deomkawe

TAZAMA PICHA ZA YALIO JIRI KATIKA HIJA YA BOKO

Hija BOKO ilikua nzuri na watu tulijifunza mengi kiroho kiukweli tumeongeza kitu katika maisha ya kiroho na maisha ya kila siku...
Kulikua na maandamano ya NJIA YA MSALABA yaliyo fuatiwa na SEMINA YA FAMILIA NA NDOA kwa vijana wote na kisha IBAA YA MISA TAKATIFU mapema saa10 tukarudi nyumbani..
MAPENDOO.....
#picha na deomkawe

Friday 13 March 2015

NJIA YA MSALABA LEO IJUMAA

Usikose kuhudhuria njia ya  msalaba leo ijuma, baada ya ibada tutandikisha kwa marayamwisho watakao enda HIJA BOKO kesho tarehe 14-3-2015 twendeni tukachote baraka.
MAPENDOOO

Tuesday 10 March 2015

TANGAZO TANGAZO JUMAMOSI TAREHE14-3-2015 TUTAENDA HIJA BOKO

Tarehe 14-3-2015 Jumamosi vijana wote tufike parokiani saa12:30 asubuhi kwa ajili ya kwenda HIJA BOKO, usafiri ni buure tutalipiwa na uongozi wa viwawa parokia.
Huko tutasali NIJA YA MSALABA itakayo anza saa3 asubuhi kisha ibaa ya MISA TAKATIFUitakayo fuatiwa na SEMINA KWA VIJANA wote..
Kwakua wengi watapend akufunga hivyo kila kijana atajitegemea katika suala la chakula hivyo hakuna gharama zozote zitakazotozwa kwa kijana yoyote yule.
TWENDENI SOTE TUKACHOTE BARAKA

Saturday 7 March 2015

MATANGAZO YA LEO JUMA PILI TAREHE8-3-2015

Tyk leo kutakua na mkutano mkuu kigangoni baruti madakuu ni HIJA BOKO na MAFUNGO PUGU wote tufike bila kukosa.
Uongozi wa parokia una watangazia vijana wotekushiriki bila kukosa HIJA ITAKAYO fanyika BOKO hija ilio anda liwa na viwawa jimbo kuu la dar-es-salaaam iatakayo fanyika jumamosi ijayo vijana wote wata ena buree yaani usafiri utalipwa na uongozi wa viwawa parokia.
TUNAWATAKIA JUMA PILI NJEMA

NOELI YA VIJANA MWAKA2014 PAROKIANI

























Hivi ndivyo mambo yalivyokua katika sherehe ya NOELI ya vijana mwaka2014 iliyo fanyika katika ukumbi wa ALAMANO parokiani UBUNGO MSEWE.
Kikundi cha burudani kili tumbuiza kama kawaida na mziki bora kabisa wa vijana ulitumika vyema kabisa kuwa buruisha vijana katika sherehe yao mambo ya likua mazuri na walipata baraka nyingi sana vija wote wa parokiani.

Thursday 5 March 2015

MAANA YA VIWAWA

Maana ya Viwawa

MAANA YA VIWAWA NA HISTORIA YA VIWAWA .
MAANA YA VIWAWA.
Viwawa maana ya Viwawa ni Vijana Wakristo Wakatoliki(Wengine wanasema ni Vijana Wakatoliki Wafanyakazi) Viwawa ni chama cha kitume cha Vijana ndani ya Kanisa ambao wanatumwa na Yesu mwenyewe kuendelea  kazi yake kwa watuwake kwamba yeye “NDIYE NJIA YA KWELI NA UZIMA”Kwa Vijana wote katika maisha yao ya kila siku.

HISTORIA YA VIWAWA KIDUNIA.
Viwawa ilianzishwa mwaka 1924 mji wa Brussel nchini Ubelgijina Padri Joseph Cardjin na kupitishwarasimi na kama chama cha kitume cha vijana Kimataifa na Balaza la Kipapa Vatican mwaka 1950.Padri Joseph Cardjin pia alianzisha YCS,hivyo VIWAWA Na YCS alianzisha yeye.Makao makuu ya VIWAWA Duniani yako Roma-Italia chini ya Rais Seraphina kutoka Korea,Katibu Mkuu Jules Adached toka Bejin,Mhazini Lisa Vaccariano toka Italia na Mratibu wa kimataifa Arniel Iway toka Philipini na mshauri Pd.Joseph Ramaguera toka Spain. 

 HISTORIA YA VIWAWA TANZANIA.
Viwawa Tanzania iliingia mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi,Jimbo kuu la Dar es salaam chini ya Mwanzilishi Padri Hendrikus Johannes Brinkhof maarufu kama Padri Mansuetus na kupitisha rasimi chama cha Kitume cha Vijana na Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) mwaka 1979.Baada ya kupitisha hapo kilitambulishwa pote Tanzania kama chama cha Vijana Wakatoriki Wafanyakazi Tanzania(VIWAWA).
Mpaka sasa chama hiki kipo kipo majimboni,kuanzia ngazi ya Jumuiya,Mtaa,Kanda,Kigango,Parokia,Kijimbo,Taifa na Kimataifa.

LENGO LA CHAMA.
      Kumuezesha Kijana awe mkristo wa kweli na raia wengine waweze kurekebisha,Kuendeleza na Kudumisha taratibu za uchumi,utamaduni,ustawi,siasa na utaalamu kufatana na mpango wa Mungukatika kutafakali injili na kusali.

      Kuunda umoja na ushirikiano kwa vijana kadili ya injili na mafundisho ya Yesu Kristo.

     Kuishi upendo wa Kikristo kama watoto wa Baba mmoja.Hii ni amri ya Yesu “Amri mpya nawapa pendaneni kama vilenilivyowapenda ninyi,nanyi mpendane vivyo hivyo.(Yoh 13:34-35).

Tuesday 3 March 2015

UPADRISHO PAROKIANI UBUNGO MSEWE

Siku ya tarehe 29-11-2014 shemasi PatricMrosso na shemasi Yohane Kimario wa shirika la wa Consolata walipata daraja la upadre parokiani ubungo msewe.

Monday 2 March 2015

LOGO YA MRADI WA MZIKI WETU

Karibuni kukodisha mziki wetu ni bora mzuri na una fanya kazi nzuri.