VIONGOZI WA PAROKIA

VIONGOZI WA PAROKIA

Sunday 26 June 2016

MATOKEO YA UCHAGUZI VIWAWA NGAZI YA PAROKIA 2016

Leo tarehe 26 . 06 . 2016 Viwawa Parokia ya Ubungo ulifanya Uchaguzi wa ngazi ya Parokia.. ambao walihusika viongozi wa kanda na vigango vyote.

Jumla ya wajumbe wote kufika kwenye uchaguzi ni 21

Kabla ya uchaguzi Mwenyekiti wa zamani aliweza kusema taharifa fupi ya uongozi wake ikiwemo: mradi wa mziki, mafungo kijimbo na kiparokia, kupata makombe ngazi ya jimbo na dekania, kuwa na timu za wachezaji (mpira wa miguu, ? Mpira wa mkono, mpira wa pete), kufanya matendo ya huruma.

Na haya ndo matokeo ya Uchaguzi wa Viwawa ngazi ya Parokia

WAJUMBE = 21

NAFASI YA MWENYEKITI (WAGOMBEA)
1.BARTAZALI FLAVIAN = KURA 6
2.INNOCENT PETER = KURA 13
3.PAULO MWAKI = KURA 2

NAFASI YA MWENYEKITI MSAIDIZI (WAGOMBEA)
1.GIDEON NESTORY = KURA 8
2.DEO MKAWE = KURA 7
3.MAGDALENA JOHN = KURA 6

NAFASI YA KATIBU (WAGOMBEA)
1.DEO MKAWE = KURA 12
2.MAGDALENA JOHN = KURA 5
3.RAPHAEL NGOMA = KURA 4

NAFASI YA KATIBU MSAIDIZI (WAGOMBEA)
1.FLAVIAN FILBET = KURA 13
2.BARTAZALI FLAVIAN = KURA 4
3.ODDO JACOB = KURA 4

NAFASI YA MWAZINI (WAGOMBEA)
1.EDSON MAFARASA = KURA 5
2. JULIA LEKADRO = KURA 13
3. VERONICA ERNEST = KURA 3

HIVYO VIONGOZI RASMI NGAZI YA PAROKIA NI HAWA HAPA

MWENYEKITI
Innocent Peter
M/MSAIDIZI
Gideon Nestory

KATIBU
Deo Mkawe
K/MSAIDIZI
Flavian Filbert

MWAZINI
Julia Lekadro

VIONGOZI HAWA WATAHAPISHWA HIVI KARIBUNI.

Friday 24 June 2016

VIWAWA UBUNGO-MSEWE NI MOTO CONSOLATA DAY 25 JUNE 2016

Aya sasa siku pendwa inawadia  Bunju katika kituo bora cha Elimu ya Dunia na Biblia Consolata mission center.

Hizi ni baadhi ya picha vijana wa msewe wakifanya yao siku moja kabla ya consolata day.. Tembelea channel yetu YouTube  VIWAWAMSEWE kujionea full video

Monday 20 June 2016

VIWAWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA DAKIKA 90 (0 - 0)

Siku ya Historia katika Parokia ya ubungo-msewe katika chama cha vijana (VIWAWA) ambako mashabiki wa Yanga Na Simba walikutana kati kati ya dimba kubwa sana MSEWE PRI STADIUM kwa dakika 90 tu.

Kila timu ilijipanga vizuri kabisa kwa ushindi Wa mabao 3 zaidi.

Meneja wa Yanga Fc Mr. Kato alisema "Simba ni watoto tu tutawafunga 15 kwa 0 leo hii pia..... (Tembelea channel yetu YouTube kusikiliza majungu hayo VIWAWAMSEWE)
Meneja wa Simba Fc Mr. Paulo alisema haya " Yanga ni watoto kwetu Na Sisi goli zetu..... (Tembelea channel yetu YouTube kusikiliza majungu hayo VIWAWAMSEWE)

Mpaka dakika 90 kuisha hakuna timu iliyochungulia lango la mwenzake kialali

YANGA:
1)kona 3
2)faulo 4
3) offside 6
4) majeruhi 2

SIMBA:
1)kona 4
2)faulo 3
3) offside 2

Saturday 4 June 2016

PICHA : TAZAMA PICHA 10 ZA SIKU YA BIRTHDAY YA TIAGO ILIYOFANYIKA PAROKIANI UBUNGO MSEWE

Kheri ya kuzaliwa TIAGO...  mmisionari Tiago mwenye hasili ya Ureno Anaye fanya kazi Tanzania parokia ya ubungo-msewe..

Tarehe 31/05 alikata keki pamoja Na viwawa Wa ubungo msewe kwa ishara ya Upendo wake Na viwawa katika parokia hii... hongera Tiago kwa siku ya kuazaliwa