VIONGOZI WA PAROKIA

VIONGOZI WA PAROKIA

Sunday, 26 June 2016

MATOKEO YA UCHAGUZI VIWAWA NGAZI YA PAROKIA 2016

Leo tarehe 26 . 06 . 2016 Viwawa Parokia ya Ubungo ulifanya Uchaguzi wa ngazi ya Parokia.. ambao walihusika viongozi wa kanda na vigango vyote.

Jumla ya wajumbe wote kufika kwenye uchaguzi ni 21

Kabla ya uchaguzi Mwenyekiti wa zamani aliweza kusema taharifa fupi ya uongozi wake ikiwemo: mradi wa mziki, mafungo kijimbo na kiparokia, kupata makombe ngazi ya jimbo na dekania, kuwa na timu za wachezaji (mpira wa miguu, ? Mpira wa mkono, mpira wa pete), kufanya matendo ya huruma.

Na haya ndo matokeo ya Uchaguzi wa Viwawa ngazi ya Parokia

WAJUMBE = 21

NAFASI YA MWENYEKITI (WAGOMBEA)
1.BARTAZALI FLAVIAN = KURA 6
2.INNOCENT PETER = KURA 13
3.PAULO MWAKI = KURA 2

NAFASI YA MWENYEKITI MSAIDIZI (WAGOMBEA)
1.GIDEON NESTORY = KURA 8
2.DEO MKAWE = KURA 7
3.MAGDALENA JOHN = KURA 6

NAFASI YA KATIBU (WAGOMBEA)
1.DEO MKAWE = KURA 12
2.MAGDALENA JOHN = KURA 5
3.RAPHAEL NGOMA = KURA 4

NAFASI YA KATIBU MSAIDIZI (WAGOMBEA)
1.FLAVIAN FILBET = KURA 13
2.BARTAZALI FLAVIAN = KURA 4
3.ODDO JACOB = KURA 4

NAFASI YA MWAZINI (WAGOMBEA)
1.EDSON MAFARASA = KURA 5
2. JULIA LEKADRO = KURA 13
3. VERONICA ERNEST = KURA 3

HIVYO VIONGOZI RASMI NGAZI YA PAROKIA NI HAWA HAPA

MWENYEKITI
Innocent Peter
M/MSAIDIZI
Gideon Nestory

KATIBU
Deo Mkawe
K/MSAIDIZI
Flavian Filbert

MWAZINI
Julia Lekadro

VIONGOZI HAWA WATAHAPISHWA HIVI KARIBUNI.

Friday, 24 June 2016

VIWAWA UBUNGO-MSEWE NI MOTO CONSOLATA DAY 25 JUNE 2016

Aya sasa siku pendwa inawadia  Bunju katika kituo bora cha Elimu ya Dunia na Biblia Consolata mission center.

Hizi ni baadhi ya picha vijana wa msewe wakifanya yao siku moja kabla ya consolata day.. Tembelea channel yetu YouTube  VIWAWAMSEWE kujionea full video

Monday, 20 June 2016

VIWAWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA DAKIKA 90 (0 - 0)

Siku ya Historia katika Parokia ya ubungo-msewe katika chama cha vijana (VIWAWA) ambako mashabiki wa Yanga Na Simba walikutana kati kati ya dimba kubwa sana MSEWE PRI STADIUM kwa dakika 90 tu.

Kila timu ilijipanga vizuri kabisa kwa ushindi Wa mabao 3 zaidi.

Meneja wa Yanga Fc Mr. Kato alisema "Simba ni watoto tu tutawafunga 15 kwa 0 leo hii pia..... (Tembelea channel yetu YouTube kusikiliza majungu hayo VIWAWAMSEWE)
Meneja wa Simba Fc Mr. Paulo alisema haya " Yanga ni watoto kwetu Na Sisi goli zetu..... (Tembelea channel yetu YouTube kusikiliza majungu hayo VIWAWAMSEWE)

Mpaka dakika 90 kuisha hakuna timu iliyochungulia lango la mwenzake kialali

YANGA:
1)kona 3
2)faulo 4
3) offside 6
4) majeruhi 2

SIMBA:
1)kona 4
2)faulo 3
3) offside 2

Saturday, 4 June 2016

PICHA : TAZAMA PICHA 10 ZA SIKU YA BIRTHDAY YA TIAGO ILIYOFANYIKA PAROKIANI UBUNGO MSEWE

Kheri ya kuzaliwa TIAGO...  mmisionari Tiago mwenye hasili ya Ureno Anaye fanya kazi Tanzania parokia ya ubungo-msewe..

Tarehe 31/05 alikata keki pamoja Na viwawa Wa ubungo msewe kwa ishara ya Upendo wake Na viwawa katika parokia hii... hongera Tiago kwa siku ya kuazaliwa

Tuesday, 31 May 2016

PICHA : TAZAMA PICHA 15 ZA MATUKIO YA KUFUNGA MWEZI WA ROZARI 31.05.2016 UBUNGO MSEWE

mwezi wa tano ni mwezi wa mama bikira maria, mama wa mkombozi, na hitimisho/kilele kilikuwa leo tarehe 31. 05. 2016 katika parokia ya ubungo msewe..


Kila fungu la rozari liliwakilishwa Na mbagala mtano ya dunia


Wednesday, 6 April 2016

MZEE MAYENJA AWASHUKURU VIWAWA WA PAROKIA YA UBUNGO MSEWE KWA UKALIMU WAO..: MATENDO YA HURUMA 14/2/2016

mnamo tarehe 14 mwezi wa 2 viwawa wa parokia ya ubungo waliamua kufanya matendo ya huruma katika nyumba ya kiongozi.. mzee wetu mayenja maeneo ya golani..

ilikuwa ni baraka kwake na kwetu vijana sababu kilikuwa ni kipindi cha kwaresma(kumbukumbu ya mateso ya kristu)  kila kijana alifurahi kumuona mzee mayenja akiwa bado yupo haueni.

mzee  mayenja ni mzee wa kanisa takribani miaka 10 katika uongozi wa kanisa.. kwa kipindi kifupi alishikwa na ugonjwa wa miguu ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kuendelea na majukumu yake..

mzee mayenja alitushukuru sana vijana lwa kusema haya "Nawashukuru vijana kwa kuja kunitembelea, Nasikia faraja kwa sababu bado mnanikumbuka katika hatua zenu, Sina cha kuwalipa ila baraka zangu zipo juu yenu, kwa kipindi hiki cha kwaresma mmefanya jambo la muhimu sana na Mungu ata wabariki sana" hayo ni maneno aliyoyasema mzee mayenja akiwa amekaa kwenye kiti chake (kama inavyo onekana kwenye picha)

Nasi kama vijana tulitoa shukrani zetu kwake na kwa Mungu  tukiwakilishwa na mwenyekiti wa Viwawa Parokia Fransic alisema  aya " Tunakushuru babu sisi ni wajuu zako wapo wengi walio tamani kuja kukuona ila kutokana na sababu mbalimbi wameshindwa ila sisi kwa umoja wetu tunawakilisha wote viwawa wa parokia ya ubungo.. Mungu atakupa nguvu utapona tu"alisema mwenyekiti wa viwawa parokia

MUNGU AKUPE NGUVU MZEE WETU MAYENJA UTAPONA TU.