mnamo tarehe 14 mwezi wa 2 viwawa wa parokia ya ubungo waliamua kufanya matendo ya huruma katika nyumba ya kiongozi.. mzee wetu mayenja maeneo ya golani..
ilikuwa ni baraka kwake na kwetu vijana sababu kilikuwa ni kipindi cha kwaresma(kumbukumbu ya mateso ya kristu) kila kijana alifurahi kumuona mzee mayenja akiwa bado yupo haueni.
mzee mayenja ni mzee wa kanisa takribani miaka 10 katika uongozi wa kanisa.. kwa kipindi kifupi alishikwa na ugonjwa wa miguu ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kuendelea na majukumu yake..
mzee mayenja alitushukuru sana vijana lwa kusema haya "Nawashukuru vijana kwa kuja kunitembelea, Nasikia faraja kwa sababu bado mnanikumbuka katika hatua zenu, Sina cha kuwalipa ila baraka zangu zipo juu yenu, kwa kipindi hiki cha kwaresma mmefanya jambo la muhimu sana na Mungu ata wabariki sana" hayo ni maneno aliyoyasema mzee mayenja akiwa amekaa kwenye kiti chake (kama inavyo onekana kwenye picha)
Nasi kama vijana tulitoa shukrani zetu kwake na kwa Mungu tukiwakilishwa na mwenyekiti wa Viwawa Parokia Fransic alisema aya " Tunakushuru babu sisi ni wajuu zako wapo wengi walio tamani kuja kukuona ila kutokana na sababu mbalimbi wameshindwa ila sisi kwa umoja wetu tunawakilisha wote viwawa wa parokia ya ubungo.. Mungu atakupa nguvu utapona tu"alisema mwenyekiti wa viwawa parokia
MUNGU AKUPE NGUVU MZEE WETU MAYENJA UTAPONA TU.